TANGAZO


Wednesday, May 16, 2012

Rais Kikwete atembelea Ofisi za Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba, Dar es Salaam leo


Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Tume ya kukusanya maoni ya Katiba, wakati alipotembelea Ofisi za Tume hiyo, jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Ndani,  jijini Dar es Salaam leo. Wakati akizungumza na wajumbe wa Tume hiyo, Rais Kikwete alirudia ahadi yake ya kuwapatia nyenzo za kazi,  ikiwemo usafiri ili kuiwezesha tume hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. (Picha zote na Freddy Maro)

Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya maoni ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba (kulia), akizungumza na Rais Jakaya Kikwete, wakati Rais alipomtembelea ofisini kwake leo. Wengine katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani (watatu kushoto), Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe (wapili kushoto) na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki.

Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Profesa Mwesiga Baregu, ambaye ni mjumbe  wa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya, wakati Rais, alipotembelea Ofisi za Tume hiyo, Dar es Salaam leo. 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Wanne kushoto Mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya kuratibu maoni  ya Katiba wakati alipotembelea ofisi za tume hiyo Jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment