![]() |
Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa |
Mei 16, 2012.
WAZIRI Mkuu wa zamani, ambaye ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa anarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya mpango wa kuboresha elimu Kata ya Kipawa, Ilala Dar es Salaam.
Hayo yalibainishwa na Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema ameandaa chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kuboresha elimu katika Kata yake ya Kipawa.
"Hafla hiyo itafanyika juni 6 mwaka huu katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Monduli Edward Lowassa"
Alisema hatua hiyo imefikiwa kufuatia juhudi zingine alizozifanya kwa ajili ya kata hiyo ambapo machi 17,2012 aliitisha matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Katika matembezi hayo mama Salma alichangia sh.milioni 3, Clouds Media Group milioni 1, wakati viongozi wa Serikali walioongozana naye walichangia sh.milioni 10 ambapo jumla yake ilikuwa sh. milioni 15.
Alisema aliguswa na jambo hilo baada ya kubaini changamoto nyingi hasa za elimu kwenye kata hiyo yenye jumla za shule za msingi 7 mbazo zinaupungufu wa madawati 5000, matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa na kutokuwa na maji.
Alisema jumla ya sh.bilioni moja zinahitajika ili kufanikisha mpango huo ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi, mashirika ya umma, Taasisi za dini, makampuni, viongozi mbalimbali na Asasi zisizoza kiserikali Ng'os kujitokeza kwenye harambee hiyo ili kufanikisha mpango huo.
Diwani Kaluwa aliwashukuru wote waliojitokeza kufanikisha matembezi ya awali na wale wanaendelea kufanikisha maandalizi ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko huo.
No comments:
Post a Comment