Diwani wa Kata ya Kipawa Ilala jijini Dar es Salaam, Bonnah Kaluwa, akizungumza katika mkutano huo, ambao alisema wataandaa chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Elimu wa Kata yake ya Kipawa Juni 6, mwaka huu, Hoteli ya Kempiski, jijini Dar es Salaam na kumtaja Wazri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa mgeni rasmi wa harambe hiyo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Said Fundi.
Diwani wa Kata ya Kipawa Ilala jijini Dar es Salaam, Bonnah Kaluwa, akifafanua jambo kwa waan dishi wa habari, wakati alipokuwa akizungumza nao kuhusu chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Elimu kwenye Kata yake ya Kipwas jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mice Masters inayoratibu harambee hiyo, Suzan Okayo.

Diwani wa Kata ya Kipawa Ilala, jijini Dar es Salaam, Bonnah Kaluwa (katikati), akizungumza na waandishi wa habari leo jijini kuhusu chakula cha hisani alichokiandaa kwa ajili ya harambee ya kuchangia mfuko wa kuboresha Elimu katika kata yake hiyo. Hafla hiyo, itakayofanyika Juni 6, mwaka huu, Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na mgeni rasmi akiwa ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Said Fundi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mice Masters inayoratibu harambee hiyo, Suzan Okayo. (Picha zote na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment