TANGAZO


Thursday, May 31, 2012

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB)


Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Rais Mstaafu wa Botswana, Festus Moghae, Rais wa Benki ya Africa, Dk. Donald Kaberuka, Mshauri wa Mfalme wa Moroco, Omar Kabbaj (kushoto), Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa (wa pili kushoto), muda mfupi kabla ya kuzindua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Afrika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 31, 2012. (Picha na Ikulu)



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akifungua mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jijini Arusha leo Mei 31, 2012 . (Picha na Mahmoud Ahmad-Arusha)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akiufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa AfDB, ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Mei 31. 2012. (Picha na Ikulu)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), akipongezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB), Dk. Donald Kaberuka (kulia), mara baada ya kumaliza kutoa hotuba ya ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Arusha leo. Katikati ni Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara. (Picha na Mahmoud Ahmad-Arusha)



Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost, Dk. Alassane Ouattara (kushoto), akibadilishana mawazo na Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Donald Kaberuka, wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Arusha leo. (Picha na Mahmoud Ahmad-Arusha)


 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais Kikwete, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mjini Arusha leo.

Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Donald Kaberuka akihutubia wakati wa  ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Arusha leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Arusha leo.


Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost, Dk. Alassane Ouattara, akihutubia wakati wa  ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Arusha leo.

Rais Kikwete akiwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Rais Mstaafu wa Botswana, Festus Moghae, Rais wa Benki ya Africa Dk. Donald Kaberuka, Mshauri wa Mfalme wa Morroco, Omar Kabbaj (kushoto), Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Marais wastaafu wa Benki ya Afrika. (Picha na Ikulu)



Rais Kikwete akiwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Rais Mstaafu wa Botswana, Festus Moghae, Rais wa Benki ya Africa Dk. Donald Kaberuka, Mshauri wa Mfalme wa Moroco, Omar Kabbaj (kushoto), Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (wa pili kushoto), wakibadilishana mawazo baada ya kupiga picha ya pamoja na Marais wastaafu wa Benki ya Afrika. (Picha na Ikulu)


Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), unavyoonekana wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa (AfDB), kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha  AICC, jijini Arusha leo.

No comments:

Post a Comment