TANGAZO


Thursday, May 31, 2012

Hasheem Thaabit atembelea Shule ya Lord Baden Powell

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell, Kanali Idd Kipingu, akizungumza wakati alipokuwa akimkaribisha mgeni wake Hasheem Thaabit (katikati), ambaye alikuwa mwanafunzi wake katika shule aliyokuwa akiiongoza ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Sekondari ya Makongo, wakati alipoitembelea shule hiyo, iliyopo Mapinga, Bagamoyo, mkoani Pwani leo. Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Pheres Magesa. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Pheres Magesa, akisalimiana na mmoja wa wanafunzi ambaye pia ni mchezaji wa mpira huo shuleni hapo, Julias Charles, ambaye anakaribiana urefu na mchezaji mpira huo wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thaabit (wa pili kulia), wakati walipofika shuleni hapo leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shule hiyo, Kanali Idd Kipingu.


Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell, Kanali Idd Kipingu, akimweleza jambo mwanafunzi wake, mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thaabit, wakati alipotembelea shule hiyo leo.


Baadhi ya wanafunzi wa Shule hiyo, wakimshangilia Hasheem Thaabit, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuitembelea.


Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Pheres Magesa, akizungumza kwa ajili ya kutoa maelezo machache ya kumtambulisha Hasheem Thaabit kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule hiyo, wakimskiliza Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Pheres Magesa, wakati alipokuwa akizungumza kwa ajili ya kutoa maelezo ya kumtambulisha Hasheem Thaabit, alipofika shuleni hapo leo mchana.

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, akimkaribisha na kumshukuru mchezaji Hasheem Thaabit kwa kufika shuleni hapo kwa ajili ya kuwatembelea. 


Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thaabit, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwatembelea leo Mei 31, 2012. Thabit, aliahidi kujenga uwanja wa mchezo huo, shuleni hapo kwa ajili ya kuviendeleza vipaji vya vijana wa shule hiyo, inayotamba katika mchezo huo nchini. Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Pheres Magesa.


Hasheem Thaabit, akielezea jambo kwa wanafunzi, wakati alipokuwa akizungumza nao, alipowatembelea leo Mei 31, 2012 na kuahidi kuwajengea uwanja wa mpira wa kikapu shuleni hapo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell, Kanali Idd Kipingu.

Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thaabit, akijibu maswali ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwatembelea leo Mei 31, 2012. Shule hiyo, inamilikiwa na aliyekuwa mwalimu wake, Kanali Idd Kipingu.


Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, ambao wengi wao ni wanachama wa Skauti, wakimuaga Hasheem Thaabit kwa kutoa ahadi ya Skauti mbele yake.


 Hasheem Thaabit, akitoa ahadi ya Skauti, wakati alipokuwa akiagwa na wanafunzi wa shule hiyo, alipomaliza kuzungumza nao wakati wa ziara yake shuleni hapo, ambapo aliahidi kuwajengea uwanja wa mpira wa Kikapu shuleni hapo. Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Pheres Magesa.


Mchezaji Mpira wa Kikapu wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thaabit (katikati), akipiga picha ya kumbukumbu na wachezaji wa mpira huo shuleni hapo, mara baada ya kukamilisha ziara yake.


Mchezaji Mpira wa Kikapu wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thaabit (kushoto), akiwaeleza jambo wacheza mpira huo shuleni hapo, mara baada ya kukamilisha ziara yake, ambapo aliwataka kuwa na juhudi katika kujifunza, kuzingatia mazoezi, nidhamu na pia kuwasikiliza walimu na kufuata mafunzo wanayofundishwa.



Mchezaji Mpira wa Kikapu wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thaabit (kushoto), akiangalia michoro ya eneo la shule hiyo, ambalo linaweza kutumiwa kwa ajili ya kukamilisha ahadi yake ya kujenga uwanja wa mchezo huo. Anayemuonesha ni Mkurugenzi wa Shule hiyo, Kanali Idd Kipingu na kulia ni Eng. Fauz Said Suleiman amabaye hujishughulisha na shughuli za ujenzi.


Mchezaji Hasheem Thaabit (kulia), akiagana kwa kupeana mikono na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, wakati alipokuwa akiondoka shuleni hapo baada ya kumalizika kwa ziara yake.

No comments:

Post a Comment