Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga akimuelekeza Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV, vinavyotayarishwa, tayari kwa kurushwa hewani.
Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez akiperuzi moja ya jarida la Burudani hapa nchini la KITANGOMA, linalochapishwa na kampuni ya Prime Time Promotions LTD.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez. Kulia ni mmoja wa watangazaji wa Clouds FM, Ruben Ndege.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga (pili kutoka kulia), akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez alieambatana na Ofisa Mahusiano wake, Alice Maro (kushoto) na kulia ni Dj Fetty.
Meneja Mkuu wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez, akifanya mahojiano mafupi na mtangazaji wa Choice FM, Thandi Kathembe (kulia) mapema jana jioni.
Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez, akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga (kulia), mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea ndani ya kampuni hiyo na kujionea mambo mbalimbali. Kushoto ni Ofisa Mahusiano wa Tigo, Alice Maro. (Picha zote na Ahmad Issa Michuzi wa www.michuzijr.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment