TANGAZO


Thursday, May 10, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal, azindua Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT),  wakati wa hafla fupi ya uzinduzi, iliyofanyika leo Mei 10, 2012, Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Mussa Juma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora), George Mkuchika (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Pius Maneno. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Tuzo ya Heshima, Ibrahim Mohamed Kaduma,  kwa kuwa Mwanachama wa Heshima wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT), wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo, Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam leo, Mei 10, 2012.


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Tuzo ya Heshima, Geoffrey Mmari kutoka Chuo cha Tumaini, Dar es Salaam kwa kuwa Mwanachama wa Heshima wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT), wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam leo.


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake, wakati akizindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), jijini Dar es Salaam leo, Hoteli ya Hyatt Regency.



Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi  na baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla ya uzinduzi huo, baada ya kuzindua rasmi wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), uliofanyika leo Mei 10, Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment