Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mussa Chang’a (mwenye suti nyeupe), kuhusu vikundi mbalimbali vya burudani vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi yake mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya mkoa wa Tabora kwa Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal. Kulia ni Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Tabora mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa, ambapo ametoa wito kwa viongozi hao, kufanya kazi kwa bidii na pia kuwahamasisha wananchi kushiriki katika sensa ya watu na makazi, itakayofanyika nchi nzima kuanzia tarehe 26 mwezi Agosti, mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa (kulia), mjini Tabora leo wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment