TANGAZO


Tuesday, May 8, 2012

Makamu wa Rais azindua Jukwa la Uchumi wa Kijani, Iringa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake, wakati alipokuwa akizindua Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea kwa siku tatu, mkoani Iringa. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 8, 2012, katika Ukumbi wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Dominic Savio, mkoani humo. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya  uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani leo, mkoani Iringa, litakaloendelea kwa siku tatu katika Ukumbi wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Dominic Savio.

Msanii wa Muziki wa Asili na Mashahiri, Mrisho Mpoto, akighani maneno yenye ujumbe Kuhusu Utunzaji wa Mazingira, mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani, uliofanyika Mkoani Iringa leo Mei 8, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, mkoani Iringa leo.

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi ya Mtakatifu Dominic Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakalofanyika kwa Siku tatu mkoani Iringa.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiufukia mti alioupanda kwa ajili ya kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi ya Mtakatifu Dominic Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, Leo Mei 8, 2012, mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment