Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi wa kituo cha Afya cha Mwera Pongwe leo, akiwa katika ziara ya Wilaya ya Kati Unguja kutembelea Maendeleo ya ya Miardi mbali mbali ya kijamii katika Mkoa wa Kusini Unguja. Ujenzi huo umefadhiliw na mwekezaji kutoka nchini Itali, Dominic Palumbo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia mashine za uchunguzi wa maradhi mbalimbali ya binadamu katika kituo cha Afya cha Mwera, Pongwe, baada ya kuweka jiwe la msingi leo, alipokuwa katika ziara ya kuona maendeleo ya miradi mbalimbali katika Mkoa wa kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Affani Othman Maalim, kuhusu matumizi ya daraja la mikoko, wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya wakulima wa Jonzani, Wilaya ya Kusini, alipokuwa katika ziara maalum ya kutembelea Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Affani Othman Maalim, kuhusu matumizi ya daraja la mikoko, alipotembelea wakulima wa Jozani, Wilaya ya Kusini, katika ziara maalum ya kukagua maendeleo ya kilimo katika Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Affani Othman Maalim, kuhusu kilimo cha umwagiliaji, alipotembelea maendeleo ya wakulima wa Bonde la mpunga la Muyuni, katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya kilimo katika Mkoa wa Kusini Unguja leo.
No comments:
Post a Comment