Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodeger Tenga (kushoto), akibadilishana hati za
makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin
Goetzsche, Dar es Salaam jana usiku, baada ya kusaini mkataba ambapo TBL
itaidhamini timu ya Taifa, 'Taifa Stars' kwa sh. bilioni 23 kwa miaka mitano.
Rais Tenga wa TFF
(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin wakitiliana saini mkataba huo jana
usiku katika Hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Michezo wa
Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Leonald Thadeo (kushoto),
akimshukuru Robin wa TBL wakati wa hafla hiyo. Katikati ni Rais wa TFF,
Leodegar Tenga.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TBL, Robin, akielezea kuhusu udhamini huo kwa Taifa Stars katika hafla hiyo, jana usiku.
Thadeo, akitoa shukrani kwa niaba ya Serikali kuhusu mkataba huo kwa Stars.
Meneja Masoko wa TBL,
Kanda ya Kusini, James Bokella (kulia), akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa
TFF, Angetile Osiah, wakati wa hafal hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin, Rais wa TFF, Tenga pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria kusainiwa kwa mkataba huo, wakifurahia jambo huku wakipata viburudisho.
Meneja wa Uhusiano wa
Mambo ya Nje na Mawasiliano wa TBL, Emma Oriyo (kulia) na rafiki yake
wakifurahia jambo wakati wa kusainiwa mkataba huo jana.
Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akipiga mpira ikiwa ni ishara ya
uzinduzi wa udhamini wa bia hiyo kwa timu ya Taifa ya soka, Taifa Stars.
Rais wa TFF, Tenga
akizungumza na mmoja wa wasanii wa kikundi cha Wanne Stars wakati walipokuwa wakitumbuiza katika hafla hiyo.
Wasanii wa kikundi cha
Wanne Stars, wakiburudisha kwa sarakasi wakati wa uzinduzi wa udhamini wa bia ya Kilimanjaro
Premium Lager kwa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment