Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi katika sherehe za kuwapongeza wananchi wa Wilaya na Mikoa kwa kuuza sana zao hilo, huko katika Uwanja wa Jamhuri Hall Wete Pemba leo.
Tuesday, April 17, 2012
Ziara ya Rais Shein Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto), akifuatana na Katibu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Alfani Othman Maalim pamoja na ujumbe aliofuatana nao katika ziara ya kutembelea bonde la Ukele, kukagua Tuta la kuzuia Maji Chumvi, katika Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba, akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya jamii wilayani humo leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Pemba)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Alfani Othman Maalim, alipotembelea bonde la Ukele, kukagua Tuta la kuzuia maji chumvi katika Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba, katika ziara hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la kituo cha Afya Chimba, Jimbo la Tumbe, alipokuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya jamii katika Mkoa wa Kaskazini Pemba leo.
Baadhi ya wananchi wa Chimba Kaskazini Pemba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la kituo cha Afya katika Shehia hiyo leo, akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya jamii mkoani humo.
Baadhi ya wananchi wa Chimba, Kaskazini Pemba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya katika Shehia hiyo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenykiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi cheti, Hamad Said Hamad, akiwa ni muuzaji bora wa zao la karafuu kwa mwaka 2012, katika sherehe za kuwapongeza wananchi walioshiriki na kuuza sana zao hilo huko katika Uwanja wa Jamhuri Hall Wete Pemba leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi cheti, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa, kwa ushindi wa Mkoa wake kushinda na kuchukua nafasi ya kwanza katika zoezi zima la uchumaji na uuzaji wa zao la karafuu kwa mwaka 2012, kwenye Shirika la ZSTC Zanzibar katika sherehe za kuwapongeza wananchi wa Wilaya na Mikoa kwa kuuza sana zao hilo, huko ukumbini Jamhuri Hall, Wete Pemba leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment