TANGAZO


Tuesday, April 17, 2012

Dk. Bilal afungua mkutano wa 26 wa wadau wa Sayansi

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dk. Mwele Malecela (watatu kushoto), kuhusu maonesho ya wanasayansi yaliyoandaliwa  na Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya magonjwa ya Binadam (NIMR), wakati alipofika kufungua mkutano wa 26 wa mwaka wa wadau wa Sayansi, ulioanza jana Aprili 16, jijini Arusha. Wa pili kushoto ni mke wake, Mama Zakhia Bilal na kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR)


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dk. Dennis Massue, wa Kituo cha Utafiti cha Amani Tanga, kuhusu vipimo vinavyofanywa na kituo hicho kwa kupima ufanisi na ubora wa viuatilifu vinavyoua mbu kwenye vyandarua kwa kutumia kifaa cha kupima ubora ‘Cone Bioassay’, wakati alipotembelea katika maonyesho ya Wanasayansi, yaliyoandaliwa  na Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya magonjwa ya Binadam (NIMR), baada ya  kuufungua mkutano wa 26 wa mwaka wa wadau wa Sayansi, ulioanza jana Aprili 16, jijini Arusha. Wa tatu kulia ni mke wake,  Mama Zakhia Bilal na wa pili ni Dk. Mwele Malecela.


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 26 wa mwaka wa wadau wa Sayansi, ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR), ulioanza jana Aprili 16, 2012 jijini Arusha, wakati akiufungua leo jijini humo.


Makamu wa Rais, Dk. Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Sayansi waliohudhuria mkutano huo wa 26 wa mwaka ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), jijini  Arusha.

No comments:

Post a Comment