Kamishna wa Ustawi wa Jamii, wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dunford Makala, akizungumza wakati alipokuwa akiifungua semina ya maadhimisho ya Siku ya Afya duniani, Dar es Salaam jana, iliyokuwa na kauli mbiu isemayo, Kuzeeka na Afya. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo cha Uelimishaji na Uboreshaji Afya, Geoffrey Kiagi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Kamishan Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo (kulia), akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina hiyo, akiwa na baadhi ya washiriki wa semina hiyo kutoka taasisi mbalimbali za kijamii nchini.
Wazee wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina hiyo, iliyokuwa na kauli mbiyu isemayo, Kuzeeka na Afya.
Baadhi ya washiriki wa semina ya maadhimisho ya Siku ya Afya duniani, wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo cha Uelimishaji na Uboreshaji Afya, Geoffrey Kiagi, akizungumza wakati wa alipokuwa akifafanua masuala kadhaa kuhusu maadhimisho ya siku hiyo, leo jijini. Kushoto ni Mshauri wa masula ya Rasilimali Watu wa Shirika la Afya, Ulimwenguni (WHO), nchini Tanzania, Dk. Martins Ovbereddjo na katikati ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii, wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dunford Makala.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dunford Makala, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, mara baada ya kuifungua semina ya maadhimisho ya Siku ya Afya duniani, inayoambatana na kauli mbiu isemayo, Kuzeeka na Afya.
Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhimiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi, akiwasilisha mada juu ya Uzee na Afya, wakati wa semina hiyo, iliyokuwa iliyowahusisha wazee na waandishi wa habari kwenye maadhimisho hayo, leo jijini.
No comments:
Post a Comment