Willium Malecela,Mgombea wa nafasi ya Ubunge Afrika Mashariki |
Katika mahojiano hayo, Mgombea Willium Malecela aliweza kuzungumzi masuala ya Ardhi na ushiriki wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hususani kwenye soko la pamoja na kuwasaidia vijana katika swala la ajira endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na Wabunge wa Jamhuri Muungano katika uchaguzi huo ili aweze kutekeleza dhamira hiyo.
Amesema dhamira yake ya kugombea Afrika Mashariki lengo lake la kwanza ni kuweza kuliwakilisha Taifa na wananchi kwa ujumla.
Aidha amewaomba waheshimiwa Wabunge wamchague ili aweze kuwa Balozi mzuri katika jumuiya hasa katika kutetea maslahi ya Taifa.
Pia ameongeza kwamba akipatiwa nafasi hiyo ataweza kuwaelimisha wananchi kuhusiana na jumuiya hiyo ili waweze kufahamu na kuielewa pamoja na majukumu yake kwa ujumla.
Pembeni katika mahojiano hayo ni Mtangazaji wa Uhuru FM Jimmy Kagaruki.(Na mpiga picha wetu Cecy Jeremiah)
No comments:
Post a Comment