Kikosi cha timu ya Simba, kilichojitupa Uwanja wa Es Setif, Algeria kupambana na timu ya Es Setif ya huko katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Washidi barani Afrika leo usiku. Es Setif imeshinda mabao 3-1 na hivyo Simba kusonga mbele kwa faida ya goli la ugenini baada ya Uwanja wa Taifa kuibamiza timu hiyo mabao 2-0 katika mchezo wa mwanzo wa hatua ya 16 bora. Goli la Simba liliwekwa kimiani na mshambuliaji wake machachari Emmnuel Okwi katika dakika ya 90, ambapo baadaye ziliongezwa daki 4 za majeruhi. Mchezaji wa Simba Senta hafu, Juma Nyosso, alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 18, tokea mchezo huo kuanza na hivyo kuifanya ngome ya Simba na timu nzima kwa jumla kuyumba na kukosa mwelekeo hadi ilipotimu dakika za 87, wachezaji walianza kutulia na kuanza kuonesha uhai kwa kulitafuta goli lililokuwa muhimu kwa timu na Watanzania wote. Mungu Ibariki Simba, Mungu wabariki Watanzania wote, popote pale walipo. Amin. (Picha, habari na Kassim Mbarouk)
Mchezaji Emmanuel Okwi, aliyewakombo Watanzania na aibu ya kufungwa mabao 3, ugenini kwa kupachika goli la dhahabu na muhimu kwa Simba na Watanzania na kuwa mabao 3-1 hadi mwisho wa mchezo huo.
Hapa Emmanuel Okwi, akionesha mbinu za kuwahadaa wachezji wa timu pinzani ya Es Setif.
Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic, akinyanyua mkono wa Okwi kumpongeza kwa juhudi zake za kuiletea Simba ushindi.
Kikosi cha Es Setif, kilichotolewa na Simba katika mashindano ya kombe hilo, leo usiku.
No comments:
Post a Comment