Mwigizaji
maarufu wa filamu nchini Steven Kanumba amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo, habari zinasema mwili wa mwigizaji huyo umepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhibili ili kufanyiwa uchunguzi na kuhifadhiwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela,
amethibitisha kutokea kifo cha mwigizaji huyo na kuongeza kwamba sababu
za kifo chake bado zinafanyiwa uchunguzi lakini taarifa za mwazo ambazo Polisi wamezipata zinasema Kanumba alikuwa na mpenzi wake chumbani na
kulitokea kutokuelewana kati yao na kusababisha kutokea kwa ugomvi
ulipelekea kifo chake. |
No comments:
Post a Comment