.y![](file:///C:/Users/kasim/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg)
![](file:///C:/Users/kasim/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg)
![](file:///C:/Users/kasim/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image003.gif)
07/04/2012
PRESS RELEASE
MASIKITIKIO JUU YA KIFO CHA MSANII
STEVEN CHARLES KANUMBA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa
masikitiko na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Msanii wa filamu Steven
Charles Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi ya Tarehe 07/04/2012
baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Sinza Vatican jijini Dar es
Salaam.
BASATA inaungana na familia za wafiwa na wasanii wote
nchini kwa maombolezo ya msiba huu
mkubwa na wa kihistoria. Kufiwa na
msanii huyu mahili kwenye tasnia ya filamu ni pengo kubwa kwa familia, Sekta ya
sanaa na Taifa kwa ujumla kutokana na ukweli kuwa, aliweza kuutangaza utamaduni
na sanaa yetu nje ya mipaka.
Kanumba atakumbukwa kwa moyo wake wa kujituma na kuthamini
kazi ya Sanaa toka akiwa Kundi la Maigizo la Kaole ambapo moyo wake huo
ulimfanya awe miongoni mwa wasanii walioleta mageuzi kwenye tasnia ya filamu
kwa kuifanya kuanza kupendwa na wadau wengi zaidi.
Aidha, atakumbukwa kwa juhudi zake za kuinua vipaji
vichanga katika tasnia ya filamu ambapo mara kadhaa katika kazi alizoziandaa
alishirikisha wasanii wachanga ambao BASATA inaamini watakuja kuwa hazina kubwa
kwa taifa letu.
BASATA linatoa pole kwa familia ya marehemu na Wasanii
wote katika kipindi hiki kigumu. Ni vema wasanii wote tukatumia kipindi hiki
kutathimini kwa pamoja michango yetu katika kukuza sekta ya Sanaa ikiwa ni
pamoja na kuimarisha umoja wetu lakini pia tukiyaenzi yale yote mema
yaliyofanywa na Steven Charles Kanumba.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba
mahali pema peponi. AMEN
Sanaa
ni Kazi Kwa Pamoja Tuikuze na Kuithamini.
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI, BASATA
![](file:///C:/Users/kasim/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image004.gif)
Barua zote
ziandikwe kwa Katibu Mtendaji
All correspondence to be addressed to
The Executive Secretary
BASATA Arts Centre, Ilala Sharif Shamba, P.O. Box. 4779, Dar es Salaam, Tanzania.
Telephone: 2863748/2860485, Fax: 0255
- (022) - 286 0486 E-mail: info@basata.or.tz Website: basata.or.tz
No comments:
Post a Comment