Mariam Hamis - Miss United Nation Zanzibar
Mariam Hamis akiwa kwenye shindano nchini Tanzania
Mariam Hamis akiwa kweye shindano nchini.
Miss Utalii Tanzania 2011, wakiwa katika Pwani ya Bagamoyo, kwenye mazoezi.
WAREMBO wawili wa Miss Utalii Tanzania 2011, watawakilisha Tanzania katika Shindano la Dunia la Miss United Nation 2012, litakalo fanyika July 28 huko Calfonia Marekani.Shindano hilo linashirikisha zaidi ya nchi 100 duniani kote.
Hii itakuwa ni fulsa nyingine ya pekee kwa nchi yetu kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania, huko nchini marekani na duniani kwa ujumla. Warembo hawa pamoja na kwenda kutangaza utalii na utamaduni wa Tanzania kwa ujumla, lakini watapeleka ujumbe mahususi kwa wamarekani na Dunia kwa ujumla juu ya mlima kilimanajaro,Seremgeti na Ngorongoro Crater kuwa viko tanzania na ni mali ya tanzania. Hii itasaidia kuondoa na kupambana na propaganda za nchi nyingine kuwa vivutio hivyo vipo kwao.
Tunafanya mpango wa kupata matilio mbalimbali kutika mamlaka ya Hifadhi za taifa (TANAPA), mamlaka ya bonde la ngorongoro (NCAA) na Bodi ya Taifa ya Utalii, za mlima kilimanjaro,serengeti na ngorongoro ikiwemo machapisho vijarida,vipeperushi, mokanda ya video,DVD na VCD zikiwa katika lugha mbalimbali, ambavyo warembo wetu watagawa kwa washiriki wa nchi zote ,na vyombo mbalimbali vya habari vya nchi hizo vitakavyo ambatana na washiriki wao,pia kupitia waandaaji hao wa dunia tutagawa katika vituo mbalimbali vya televisheni na magazeti nchini marekani.
Aidha mchakato wa kupata wadhamini wa kugharamia safari na ushiriki huo umeanza na unaendelea vizuri.
Mariamu Hamisi ni mshindi wa Miss Utalii Dodoma 2011 na mshindi wa taifa wa tuzo ya Miss Utalii tanzania 2011 - Gender,wakati Evamary Gamba ni mshindi wa Miss Utalii tanzania Kilimanjaro 2011 na mshindi wa Taifa wa tuzo ya Miss Utalii Tanzania 2011 - Mount Kilimanjaro. Matarajio ya kutwaa taji ni makubwa kutokana na ukweli kuwa washiriki wetu wanakidhi matakwa na kanuni za kushiriki na kushinda taji la Miss United Nation World.
Kabla ya kuondoka warembo hawa watafanya ziara za mafunzo kati hifadhi za Kilimanjaro,Ngorongoro na Serengeti, kwani ndo ajenda na kipaumbele cha ushiriki wetu katika mashindano hayo mwaka huu. Aidha bodi ya maandakizi ya Miss utalii tanzania ,imepitisha kuwa washiriki wote wa Miss Utalii tanzania katika mashindano ya kimataifa na dunia watatumia ligha ya kiswahili ,stejini ili kukitangaza kiswahili, kama ambavyo mataifa na washiriki wa mataifa mengine wamekuwa wakitumia lugha za nchi zao na kushinda mataji.
Miss Tourism Tanzania Symbol Of National Heritage - Do Value Added Pageant
"Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Living'
No comments:
Post a Comment