Rais wa Sudan , Omar al-Bashir, ametupilia mbali uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini, kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa na wanajeshi wake ndani ya Sudan Kusini.
Bashir amesema jirani wake huyo hakuonyesha nia ya amani na kwamba utawala wa Juba unaamini na vita.
Rais Al Bashir amesema haya wakati akizungumza na wanajeshi wake katika eneo la Heglig, ambalo lilitekwa na wanajeshi wa Sudan Kusini kwa siku kumi.
Tayari wanajeshi wa Sudan Kusini wameondoka eneo hilo
Katika maiezi ya karibuni, kumekuwepo na makabiliano kati ya pande mbili kwenye maeneo yanayozalishwa mafuta ambayo huwa katika mpaka unaozozaniwa, hali iliyozua wasi wasi ya kuzuka kwa vita.
Rais wa Marekani Barack Obama amezitaka nchi hiyo kuanza mazungumo na kumaliza tofauti zao kwa amani.
No comments:
Post a Comment