Msanii Bob Junior, akiwapagawisha mashabiki, msanii huyo, alipokuwa akishirikiana na makundi ya Wasanii Marlaw, Amini, Khadija Kopa, bendi ya Akudo Impact na Tip Top Connection, kutoa burudani kwenye ukumbi wa Kisasa wa Dar Live, Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo na kufunika vilivyo kwa nyimbo na shoo zao za nguvu ndani ya Ukumbi huo. (Picha Zote na Richard Bukos/GPL)
Msanii Amini akilitawala jukwaa la Dar Live huku mashabiki wakimshangilia.
Kiongozi wa Akudo Impact, Christian Bella, akionesha ufundi wake wa kuimba na kulitawala jukwaa, wakati wa burudani hiyo ya pamoja.
Msanii Tunda Man, akiwapa tano mashabiki wake kwa kumkubali kweli kweli katika burudani alililokuwa akiliporomosha kwenye ukumbi huo.
Msanii Marlaw, akiwapagawisha wapenzi wa burudani ndani ya Dar Live kwa miondoko ya kuzirudi ngoma kiduku kiduku, kama anavyoonekana katika shoo hiyo pichani.
Naye mama Malkia wa mipasho nchini, Khadija Kopa akiwadatisha wapenzi wa taarab, waliokuwa wamefurika ukumbini humo, usiku huo.
Dogo Janja wa Tip Top Connection, akiwapeleka puta mashabiki wake katika onesho hilo la pamoja.
Nao, akina dada wanenguaji wa bendi ya Akudo Impact, waliwarusha roho mashabiki ile mbaya kwa shoo zao za uhakika na za ukweli kama inavyoonekana katika picha hii.
Hawa nao ilikuwa balaa, Ma DJ, walikuwa wakizimwaga ngoma za uhakika ambazo ziliwafaya wasanii pamoja na mashabiki wao kuhemkwa kila mara kwa kuimba na kuzirudi ngoma hizo, ukumbini humo.
No comments:
Post a Comment