Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhani Khijjah, akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini leo, kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika Kitaifa mwezi Agosti mwaka huu, wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea, jijini Dar es Salaam. (Picha na Aron Msigwa- MAELEZO)
Baadhi ya viongozi wa dini wanaoendelea na mkutano wao, jijini Dar es Salaam, wakipitia vitabu na vipeperushi, vyenye ujumbe mbalimbali, kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi, litakalofanyika nchini, mwezi Agosti mwaka huu, baada ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa semina fupi kuhusu ushiriki wa viongozi hao katika kufanikisha sensa hiyo.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini, wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhani Khijjah, alipokuwa akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi 2012 na namna Serikali ilivyojipanga kulifanya zoezi hilo kwa ufanisi.
Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa, akisisitiza jambo kuhusu sensa ya watu na makazi, itakayofanyika mwaka huu, wakati wa semina ya viongozi wa dini jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhani Khijjah (kushoto), akiandika maswali yaliyoulizwa na viongozi wa dini, kuhusu namna Serikali ilivyojipanga kufanya sensa ya watu na makazi, itakayofanyika mwezi Agosti 2012. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa (katikati) na Kamishna wa Sensa, Hajjat Amina Mrisho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhani Khijjah (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa, wakati wa mkutano wa viongozi wa dini, unaoendelea jijini Dar es salaam. Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekutana na viongozi hao kufuatia umuhimu na ushawishi wao katika jamii, ili waweze kushiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi hilo, litakalofanyika mwezi Agosti 2012.
No comments:
Post a Comment