Tangi la maji safi na salama, lililojengwa katika shehia ya Ziwani, Wilaya ya Chake chake kisiwani Pemba. Tangi hilo linauwezo wa kubeba maji lita 250,000 na urefu wa mita 18. Ujenzi wa tangi hilo, umefadhiliwa na Japan pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ambapo wananchi wapatao 17,000, watafaidika na mradi huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi wa Shehia ya Ziwani na vijiji jirani, wakati wa ufunguzi wa tangi la maji, Ziwani, wilayani Chake chake, Pemba, akiwa katika ziara yake hiyo, kisiwani humo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifunua pazia, kuashiria ufunguzi wa tangi hilo la maji la Ziwani leo, katika ziara yake ya Mkoa wa Kusini, kisiwani Pemba.
Baadhi ya wananchi wa Shehia ya Ziwani na vijiji jirani, wakimsikiliza, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokua akizungumza nao wakati wa shereheza ufunguzi wa tangi la maji la Ziwani, Wilaya ya Chake chake Pemba leo.
No comments:
Post a Comment