TANGAZO


Friday, April 20, 2012

Rais Shein akutana na kikosikazi cha uvunaji karafuu kisiwani Pemba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi ambao ni Wajumbe wa Kikosi cha 'Task Force', ya Taifa, kuhusu ufanikishaji wa uvunaji wa zao la karafuu, alipowasili katika Viwanja vya  Kiwanda cha Makonyo, Jimbo la Wawi, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini kisiwani Pemba leo. (Picha na Ramadhan Othman, Pemba)



Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Thuwaiba Edington Kisasi, akimkabidhi zawadi, Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ikiwa ni tunzo ya karafuu ya mwaka 2011-2012 katika mkutano wa ufungaji wa msimu wa zao hilo, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kiwanda cha Makonyo, Wawi Pemba.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kikosi kazi cha Taifa, kilichoshughulikia uvunaji na uuzwaji wa zao la karafuu, kisiwani Pemba katika ukumbi wa  kiwanda cha makonyo, Wawi Pemba. Rais ameufunga msimu wa zao hilo wa mwaka 2011-2012 leo, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi kazi (Task Force) cha Taifa cha uvunaji wa zao la karafuu huko kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chake-chake, kisiwani Pemba , akiwa katika ziara yake mkoani humo leo.

No comments:

Post a Comment