Wanajumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, wakicheza moja ya ngoma za Kiganda wakati wa tamasha leo hilo.
Wasanii Narayenga Annet (kulia), Ritah Nasaka (kushoto) na Hawa Nakalanzi, wakionesha jinsi mwanamke wa Kiganda anavyotakiwa avae, mavazi ya heshima wakati wa kuonesha sanaa ya nyimbo na maigizo kwenye tamasha hilo.
Wasanii Narayenga Annet (kulia), Ritah Nasaka (kushoto) na Hawa Nakalanzi, wakifurahia mavazi yanayotakiwa kuvaliwa na mwanamke wa Kiganda wakati wa kuonesha sanaa hiyo, kwenye tamasha hilo.
Wanajumuiya ya watu wa Uganda waishio Tanzania, wakionesha kukubali kuvutwa na wenzao wa timu pinzani katika mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume.
Wanajumuiya wa kike wakivutana na kamba katika mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake kwenye tamasha hilo la Uganda family Day, viwanjani hapo.
Baadhi ya wanajumiya ya wananchi wa Uganda, waishia Tanzania, wakikimbiza kuku katika mchezo wa kukimbiza kuku wakati wa tamasha hilo. |
Kijana aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Ismail, akiwa na kuku wake aliyemkamata wakati wa mashindano ya kukimbiza kuku kwenye tamasha hilo.
Baadhi ya wanajumuiya, wakicheza moja ya ngoma za Kiganda zilizokuwa zikipigwa kwenye tamasha hilo.
Baadhi ya watoto wa wanajumuiya, wakicheza huku wazazi wao wakishiriki kwenye michezo mbalimbali kwenye tamasha lao hilo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma (kulia), akicheza na wasanii waliokuwa wakicheza moja ya ngoma za asili ya Waganda, iliyokuwa ikipigwa viwanjani hapo. |
Msanii Hawa Nakalanzi, akionesha ustadi wake wa kuzicheza ngoma za asili ya Kiganda zilizokuwa zikipigwa kwenye tamasha hilo.
Baadhi ya wanajumuiya, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye tamasha hilo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma (JB), akizungumza wakati akilifunga tamasha hilo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma (JB), akimtambulisha mmoja wa wanajumuiya hiyo, Opherus Musasira, ambaye ameishi nchini Tanzania zaidi ya miaka 20, kwa wanajumuiya hao.
No comments:
Post a Comment