Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akipita mbele ya dimbwi la maji yaliyotuama kwenye mitaa ya Serikali ya mtaa wa Karume leo asubuhi, wakati alipokuwa akifanya ukaguzi wa mazingira kwenye mitaa ya eneo hilo.
Wakazi wa maeneo ya Serikali ya mtaa wa Karume, wakiangalia moja ya dimbwi la maji yaliyotuama kwanye eneo lao hilo, wakati Mbunge wao, Mussa Azzan 'Zungu', alipofanya ukaguzi wa mazingira katika mitaa ya Serikali hiyo leo.
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' (katikati), akiwa pamoja na wananchi wa Serikali ya mtaa wa Karume, kuangalia moja ya madimbwi ya maji yaliyosababishwa na kuziba kwa chemba za maji taka kwenye mtaa wa Saadan, Ilala jijini Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akifanya ukaguzi wa mazingira katika eneo hilo.
Magari yakipita mtaa wa Lindi leo, ukiwa umejaa maji ya mvua, ambao ni mmoja wa mitaa ya Serikali ya mtaa wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akipatiwa maelezo kuhusu kutuwama kwa maji na sababu zinazo sababisha kutuwama huko, wakati alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa mazingira katika eneo la Serikali ya mtaa wa Karume, Dar es Salaam leo asubuhi.
Mhadisi wa Manispaa ya Ilala. Eng. Ogare Salu Charles, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu hatua wanazokusudia kuzichukua, kuondoa matatizo ya kuziba kwa mifereji kunakopelekea kufurika na kutuwama kwa maji kwenye maeneo ya Serikali ya mtaa wa Karume, baada ya kufanya ukaguzi huo na Mbunge Zungu (kulia), leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment