TANGAZO


Thursday, April 19, 2012

Tamasha la ngoma za asili kuadhimishwa Songea

 Msanii Peter Komba, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati Kamati ya maandalizi ya Tamasha la ngoma za Utamaduni wa makabila ya Mkoa wa Ruvuma, kutoka Kituo cha Habari na Maendeleo ya Vijana cha Makangarawe, walipokuwa wakizungumza nao, Dar es Salaam jana, kuhusu tamasha hilo, litakalofanyika Aprili 27 hadi 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea mkoani humo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kituo hicho,  Julius Mkada na Katibu wake Hashim Polwe. (Picha zote na Kassim Mbarouk)




 Msanii Peter Komba, akiwaonesha waandishi wa habari, moja ya vifaa vinavyotumiwa na makabila ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma, wakati wa mkutano huo, leo mchana. Kulia ni Mwenyekiti wa Kituo hicho,  Julius Mkada na Katibu wake Hashim Polwe. 




 Msanii Mose Francis 'Dollo' wa Wanaume Halisi, ambao watashiriki katika tamasha hilo, mkoani humo, akirapu, wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo. Kulia ni msanii Jumanne Omary 'JB Mkuu wa Majaji' na Rashid Ziad 'KR', wote wa kundi hilo.




 Msanii Rashid Ziad 'KR', akirapu wakati wa mkutano huo. Kushoto ni msanii Mose Francis 'Dollo' na kulia ni Jumanne Omary 'JB Mkuu wa Majaji', wote wa kundi hilo. 


Msanii Jumanne Omary 'JB Mkuu wa Majaji', akionesha ufundi wake wa kurap kwenye mkutano huo. Kushoto ni wasanii Dollo na KR wa kundi hilo.

No comments:

Post a Comment