Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akikata utepe, ikiwa ni ishara ya kuzindua mfumo wa malipo ya michango ya wanachama wa GEPF kwa kupitia huduma ya Airtel money katika hafla iliyofanyika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza leo. Kushoto ni Meneja wa kitengo cha Airtel money, Asupya Nalingingwa, akifatiwa na Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi, Ladislaus Salema. (Picha na Mpigapicha wetu)
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akikata utepe wa uzinduzi wa mfumo wa malipo ya michango ya wanachama wa GEPF, kupitia huduma ya Airtel money katika hafla ya uzinduzi uliofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Airtel money, Asupya Nalingingwa, Naibu Waziri wa Fedha Gregory Teu na Kaimu Mwenyekiti wa bodi, Ladislaus Salema. Kulia ni Menaja Masoko wa GEPF, Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikiro.
Meneja wa Kitengo cha Airtel money, Asupya Nalingingwa, akimshukuru Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, mara baada ya kuzindua mfumo wa malipo ya michango ya wanachama wa GEPF kwa kupitia huduma ya Airtel money, uzinduzi huo ulifanyika katika Hotel ya Golden Crest Mwanza. Wengine pichani ni viongozi na wajumbe wa GEPF pamoja wageni mbalimbali walioshiriki uzinduzi huo.
Meneja wa kitengo cha Airtel money, Asupya Nalingingwa, akiongea na waandishi wa habari, leo jijini Mwanza, wakati alipokuwa akifafanua kuhusu mfumo maalumu wa malipo kupitia Airtel Money, utakaowawezesha wanachama wa GEPF kulipa michango yao ya mwenzi.
No comments:
Post a Comment