TANGAZO


Wednesday, April 18, 2012

Chelsea 1 Barcelona 0


Didier Drogba
Drogba aizamisha Barcelona katika nusu fainali ya klabu bingwa mkondo wa kwanza
Didier Drogba aliishangaza Barcelona alipofunga bao la Chelsea, na la pekee, katika mechi dhidi ya Barcelona, na kuiongezea timu yake matumaini ya kufika katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.
Drogba alifunga katika kipindi cha kwanza, baada ya dakika mbili kuongezwa, huku vijana wa meneja wa Chelsea, Roberto di Matteo wakiimarisha ngome kali katika uwanja wao wa Stamford Bridge.
Barcelona waliumiliki mpira daima katika mechi hiyo, lakini walishindwa kumpita kipa wa Chelsea, Petr Cech.
Mara mbili Barcelona waligonga mwamba, lakini kweli bahati haikuwa yao.
Hayo yalimpata Alexis Sanchez katika kipindi cha kwanza, na baadaye naye Pedro akitumaini kufunga bao la chini kwa chini, hakufanikiwa, na baadaye mkwaju wake pia ukigonga mwamba.
Kiungo cha kati wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas, naye alielekea kufunga, lakini mpira ukaokolewa na Ashley Cole kabla tu ya kuingia wavuni.
Ingawa Chelsea imefanikiwa kuongoza mkondo wa kwanza wa nusu fainali baada ya timu hizo kukutana Jumatano jioni, bila shaka wachezaji hao wa timu ya England wanafahamu watakuwa na kibarua kigumu katika uwanja wa Nou Camp wiki ijayo katika mkondo wa pili.

No comments:

Post a Comment