Nyaraka za siri zilizonakiliwa na Ukoloni wa Uingereza na ambazo zilidhaniwa kupotea zimetolewa na serikali hiyo. Mwaka uliopita serikali ya Uingereza iliwasilisha hoja mahakamani kupinga kutolewa kwa nyaraka hizo.
Baadhi ya matukio kwenye nyaraka hizo ni pamoja na harakati za vugu vugu la ukombozi wa uhuru wa Kenya Mau Mau, kutwaaliwa kwa Kisiwa cha Chagos ambapo jamii asilia zilihamishwa pamoja na hali ya hatari katika Kisiwa cha Malaya.
Wizara ya mambo ya nje imesema inatoa taarifa zote licha ya hatua za awali kuziweka nyaraka hizo kama habari maalum. Hata hivyo wanazuoni wamehoji wakati wa kutolewa kwa nyaraka hizi na kutilia shaka uhakiki wake.
Baadhi ya habari kwenye nyaraka hizo ni;
· Hofu ya utawala wa Ki-Nazi kushambulia Afrika Mashariki mwaka 1930,
· Sheria ya kutwaa mifugo wa raia wa Kenya walioshukiwa kuunga mkono harakati za kundi la Mau Mau miaka ya 50.
· Mpango wa siri wa kumpeleka uhamishoni kiongoni wa jamii ya Wagiriki kisiwani Cyprus hadi Ushelisheli licha ya kufanya mazungumzo naye kumaliza maasi kisiwani Cyprus mwaka wa 1955.
· Harakati za kuwaondoa jamii asilia katika kisiwa cha Chagos kilizotangazwa kama himaya ya Uingereza.
· Hofu ya kuchochea chuki za rangi miongoni mwa wanafuzi kutoka Kenya walijiunga na vyuo nchini Marekani mwaka 1959 ambao babake rais wa Marekani Barack Obama alijiunga na Chuo Kikuu huko Hawaii.
Hapo Januari mwaka 2011, katika kesi iliyowasilishwa na wakenya wanne walioshiriki harakati za Mau Mau, serikali ya Uingereza ililazimika kukiri kupokea nyaraka za siri 8,800 kutoka kwa maafisa wake walitawala kolini za Uingereza, kabla ya nchi hizo kupata uhuru.
No comments:
Post a Comment