Sunni Muslim Jamaat, wamlalamikia Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Nahodha, kukiuka taratibu
Mwanajumuiya ya Sunni Muslim Jamaat, Sheikh Majid Saleh, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu mgogoro wa Msikiti wa Jumuiya hiyo, uliopo mtaa wa Masque karibu Msikiti wa Ibadhi na mtaa wa Indira Gadhi, walipokuwa wakimlalamikia Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kwa kuuingilia kati na kusababisha kukiukwa kwa taratibu zao, kiimani pia kutengua uongozi halali uliokuwepo na kuweka uongozi mpya kinyume cha taratibu. (Picha na Kassim Mbarouk)
Wanajumuiya ya Sunni Muslim Jamaat, wakimsikiliza, Sheikh Maggid Saleh, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kadhia hiyo.
Mmoja wa wanajumuiya ya Sunni Muslim Jamaat, Muhammad Khatri, akiafanua jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam, leo asubuhi.
Mwanajumuiya ya Sunni Muslim Jamaat, Mjumbe wa Bodi, Mohamad Jalal Shariff, akifanua jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, jijini leo.
Sheikh Majid Saleh, akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakichukua maelezo na picha za Sheikh Majid Saleh na wanajumuiya hao, wakati mkutano huo.
No comments:
Post a Comment