Baadhi ya wanashirikisho la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vyuo Vikuu, wakiwa na mabango yao yenye ujumbe tofauti, wakimsubiri Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, ili wawasilishe ujumbe wao kwake.
Wanashirikisho wakionesha ujumbe uliokuwemo kwenye bango lao, nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanashirikisho la CCM, Vyuo Vikuu, wakiimba nyimbo za Chama hicho wakati wakimsubiri Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, ili wawasilishe ujumbe wao kwake.
Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, akisoma mabango ya Shirikisho la Chama hicho, Vyuo Vikuu nchini, walipoandamana hadi Ofisi Ndogo ya Makao Makuu, Lumumba, jijini kupeleka ujumbe wao wa kuwaunga mkono Wabunge na Kamati Kuu ya CCM, kumtaka Rais Jakaya Kikwete, kuwawajibisha wabadhirifu wa mali za Umma haraka.
Mwenyekiti wa Shirikisho la CCM, Vyuo Vikuu nchini, Asenga Abubakar, akisoma risala yao baada ya Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, kuwapokea ofisini hapo leo mchana.
Mwenyekiti wa Shirikisho la CCM, Vyuo Vikuu nchini, Asenga Abubakar, akielezea mambo mbalimbali ambayo watayatelekeza, ikiwa hatua ya kuwawajibisha wabadhirifu hao itachelewa kuchukuliwa. Nyuma yake kushoto ni Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, akisikiliza maelezo hayo.
Baadhi ya wanashirikisho la CCM, Vyuo Vikuu, wakifurahi wakati wakimsikiliza Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza nao, nje ya Ofisi ya Chama hicho leo mchana.
Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza nao.
No comments:
Post a Comment