Baadhi ya Maraisi wa Vyama vya mchezo wa Masumbwi nchini wakiangalia mpambano wa kuwania Ubingwa wa IBF Afrika kati ya mabondia Mada Maugo na Francis Cheka, kwenye ukumbi wa PTA, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam jana usiku.
Mpambano wa utanguli: Ibrahimu Maokola (kulia), akipambana na Saidi Mbelwa katika pambano la utangulizi kabla ya mabondia Mada Maugo na Francis Cheka kupanda ulingoni. Bondia Maokola alishinda kwa Point. (Picha na zote na Super D, Mnyamwezi)
Baadhi ya waamuzi kutoka nje ya nchi, wakisubiri kuchezasha mpambano wa ubingwa wa IBF Afrika kati ya mabondia Mada Maugo na Francis Cheka jana.
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wamekaa katika VIP, wakifuatilia mpambano wa mabondia hao.
Mada Maugo (kushoto), akijaribu kukwepa konde la mkono wa kulia la Francis Cheka.
Francis Cheka (kushoto), akimtupia ngumi ya mkono wa kushoto Mada Maugo, iliyokwenda hewani bila mafanikio.
Bondia Francis Cheka akivalishwa mkanda na mgeni rasmi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jery Slaa, mara baada ya bondia Mada Maugo kukataa kuendelea na mchezo na hivyo Cheka kuibuka bingwa wa pambano hilo.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jery Slaa, akimkabidhi funguo ya gari, bondia Francis Cheka baada ya kuibuka bingwa wa K.O ya raundi ya 6 jana.
No comments:
Post a Comment