Wachezaji wa JKT Ruvu, wakiomba dua kabla ya mpambano wao na Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mashabiki wa Simba, wakishangilia goli la kwanza la timu hiyo, lililofungwa na Uhuru Suleimani.
Mchezaji Kessy Mapande wa JKT Ruvu, akimtoka Emmanuel Okwi wa Simba, katika mchezo huo.
Haruna Moshi wa Simba (mbele), akipambana na Kessy Mapande wa JKT Ruvu.
Gervais Kago wa Simba (kushoto), wakikimbilia mpira na Hassan Kikutwa wa JKT Ruvu.
Haruna Mushi, akimtoka George Minja wa JKT Ruvu, kuelekea langoni mwa timu hiyo.
Wachezaji Patrick Mafisango (mbele) na Haruna Moshi, wakishangilia goli, baada ya Haruna kuifungia timu yake ya Simba goli la pili katika mchezo huo. Nyuma ni Gervais Kago wa timu hiyo.
Haruna Moshi akipiga shuti mbele ya George Minja wa JKT Ruvu.
Golikipa Juma Kaseja wa Simba, akiokoa mpira wa kono ulioelekezwa golini kwake, wakati wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment