Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff, alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre, kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Open Government Partnership, ukibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012. Kutoka kushoto ni Waziri katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Maalim na Mshauri wa Rais (Masuala ya Siasa) Dk. Laurian Ndumbaro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa meza kuu na mwenyeji wake Rais wa Brazil, Mama Dilma Rousseff na wajumbe wengine katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani, Mama Hilary Clinton.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa meza kuu na mwenyeji wake Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff, pamoja na wajumbe wa nchi mbalimbali katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, katika mkutano huo. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani, Mama Hilary Clinton.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, katika mkutano wa Open Government Partnership.
Wajumbe wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na kiraia, wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana.
Baadhi ya wajumbe wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na kiraia, wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia.
Wajumbe wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na kiraia, wakiwa pamoja na wajumbe wa nchi nyingine kwenye mkutano huo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea na Waziri Mkuu wa Georgie, Nika Gilauri katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre, jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012 baada ya kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership.
No comments:
Post a Comment