Wednesday, April 18, 2012
Airtel yakabidhi kompyuta UDOM
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akikabidhi moja kati ya kompyuta 20, zilizotolewa na Airtel kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula (kulia), wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo chuoni hapo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa. Airtel imetoa vitabu 104 na kompyuta 20 kwa chuo hicho, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 25, ikiwa ni muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando, akikabidhi baadhi ya vitabu vilivyotolewa na Airtel kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula (kulia), wakati wa hafla ya makabidhiano, iliyofanyika leo, chuoni hapo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, Betty Mkwasa.
Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM), Profesa Idrisa Kikula, akiwashukuru Airtel, wakati wa hafla hiyo, baada ya kukabidhi vitabu 104 na kompyuta 20, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 25 kutoka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa, akiongea mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya wanafunzi wa Chuo hicho (hawapo pichani), wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20, chuoni hapo leo. Vifaa hivyo, vinathamani ya sh. milioni 25. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa, akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), leo pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi wa IT wa chuo hicho, wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 25.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment