Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake, wakipata maelezo kuhusu Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Brazilian Agriculture Research Enterprise - EMBRAPA), walipoitembelea taasisi hiyo, Aprili 17, 2012, nje kidogo ya jiji la Brasilia. (Picha zote na Ikulu)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akijaribu kofia aliyopewa kama zawadi na uongozi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Brazilian Agriculture Research Enterprise - EMBRAPA), alipoitembelea taasisi hiyo, nje kidogo ya jiji la Brasilia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akipata maelezo kuhusu mashine ya kisasa ya kutambua muda wa kumwagilia maji shambani, iliyoundwa na Taasisi hiyo ya Utafiti wa Kilimo, alipoitembelea na ujumbe wake, nje kidogo ya jiji la Brasilia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu ukulima wa nyanya wa kisasa katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Brazilian Agriculture Research Enterprise - EMBRAPA), walipoiitembelea April 17, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakioneshwa mazao ya ukulima wa nyanya wa kisasa katika taasisi hiyo, walipoitembelea, nje kidogo ya jiji la Brasilia.
No comments:
Post a Comment