TANGAZO


Wednesday, April 18, 2012

Dk Bilal afungua maonesho ya Vyuo Vikuu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo, kutoka nje ya Global Education Link, Abdulmalik Mollel, wakati alipotembelea banda la Uwakala huo wa Vyuo nchini kwenye Maonesho ya Taaluma ya Vyuo Vikuu vya Elimu ya Juu nchini, Dar es Salaam mara baada ya kuyafungua maonesho hayo leo. Kushoto ni  Rahul Gupta Mwakilishi wa Chuo cha  MMu. (Picha na Mpiga picha Wetu)




Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka nje ya Global Education Link, Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya taaluma ya Vyuo Vikuu vya Elimu ya Juu, Dar es Salaam leo, mara baada ya kuyafungua maonesho hayo. Katikati ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawabwa.






Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal,  akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka nje ya Global Education Link, Abdulmalik Mollel, kuhusu shughuli zinazofanywa na mtandao huo wa Uwakala wa Vyuo vya Nje, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya Vyuo, kwenye maonesho ya Taaluma ya Vyuo Vikuu vya Elimu ya Juu, Dar es Salaam leo, mara baada ya kuyafungua maonesho hayo.  Katikati ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawabwa.

No comments:

Post a Comment