Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao katika mkutano wa majumuisho ya ziara yake, aliyoifanya katika Wilaya hizo zilizo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika leo kwa mkutano huo, ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete. (Picha na Ramadhan Othma, Pemba)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, katika mkutano wa majumuisho ya ziara yake mkoani humo. Katikati ni Waziri wa Bishara, Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui.
Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao katika mkutano wa majumuisho ya ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba leo.
Baadhi ya Viongozi hao, wakiwa katika mkutano wa majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, kisiwani Pemba leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Msikiti wa Masjid Raudha, katika kijiji cha Kiuyu Maungweni, Jimbo la Ole, Mkoa wa Kaskazini Pemba leo, alipofanya ziara katika kijiji hicho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Shehia ya Kiuyu, Maungweni, Jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba leo, baada ya kuufungua Msikiti wa Masjid Raudha, kijijini hapo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akiwasalimia waumini wa Dini ya Kiislamu, baada ya kuwapa nasaha zake wakati alipouzindua Msikiti wa Masjid Raudha, katika kijiji cha Kiuyu Maungweni Ole, Kaskazini Pemba leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Watoto mara baada ya kuzindua Msikiti wa Masjid Raudha katika shehia ya Kiuyu Maungweni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika upandaji wa miche ya Mikarafuu, katika shamba la Mikindani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba leo, akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo, mkoani humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi wa Chama hicho, alipowasili katika uwekaji wa jiwe la msingi wa tawi la CCM Tumbe, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo. (Picha na Ramadhan Othman, Pemba)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi wa Tawi la CCM, Kinyasini, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi wa chama, alipowasili katika uwekaji wa jiwe la msingi Tawi hilo kijijini hapo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi wa na wanachama Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Tumbe, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba alipofanya ziara ya kuimarisha Chama katika Wilaya hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi pamoja na wanachama cha Mapinduzi wa Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ziara yake hiyo.
No comments:
Post a Comment