Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama (katikati), akizungumza na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM, Philip Mangula (kushoto) na Yussuf Makamba, wakati wa shughuli za maziko ya aliyekuwa Ofisa Mwandamizi, Makao Makuu ya CCM, Gordon Mwakitabu, mjini Dodoma leo.
Mjane wa Gordon Mwakitabu, Janeth Mwakitabu, akiangua kilio wakati wa kuuaga mwili wa marehemu mumewe, leo nyumbani kwao, Area C, mjini Dodoma.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Mwakitabu wakati wa kuaga mwili wake.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akiaga mwili wa marehemu Mwakitabu, nyumbani kwa marehemu, Area C, mjini Dodoma leo.
Makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Philip Mangula wakiuaga mwili wa marehemu Mwakitabu.
Waombolezaji wakiwa katika huzuni na mshangao, wakati wa kuaga mwili wa marehemu Mwakitabu. Waliokaa mbele, kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Mambo ya Nje, Januari Makamba, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Chiligati.








No comments:
Post a Comment