Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, akiwapungia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na mke wa muasisi wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu J.K Nyerere, Mama Maria Nyerere, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe za miaka 48 ya Muungano katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, alipokuwa akiingia kwenye Uwanja huo, tayari kwa sherehe hizo.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, akikagua kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kabla ya kuanza gwaride la maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, akikagua kikosi cha Jeshi la Magereza wakati wa gwaride la maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Viongozi wa Kitaifa pamoja na wastaafu, wakiwa wamesimama, wakati Rais Jakaya Kikweteni, akikagua vikosi vya Jeshi kwa ajili ya gwaride la maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais Jakaya Kikwete, akikagua kikosi cha Jeshi la Magereza (wanawake ), wakati wa maadhimisho hayo. (Picha na Richard Mwaikenda)
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wake, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipofika jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012, katika sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye jukwa hilo katika maadhimisho hayo.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na mke wake, Mama Salma Kikwete, wakati wa maadhimisho hayo leo jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, katika maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na mjane wa Mwasisi wa Muungano, Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hayati, Abeid Aman Karume, Mama Fatma Karume kwenye sherehe hizo za maadhimisho ya mika 48 ya Muungano wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Uwanja wa Uhuru katika sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano, jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na mke wa muasisi wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu J.K. Nyerere, Mama Maria Nyerere, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika maadhimisho hayo. (Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange (katikati) na Makamu wa wake, Dk Bilal wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika maadhimisho hayo.
Viongozi wa Kitaifa, wakiwa wamesimama jukwaa kuu pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali, wakati wimbo wa Taifa ukipigwa, uwanjani hapo.
Baadhi ya wananchi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo, wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye maadhimisho hayo.
Wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakiwakazini kuchukua matukio wakati w maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi, Uwanja wa Uhuru jijini.
Kikosi cha Jeshi la Wanamaji, kikitoa heshima zake kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais Jakaya Kikwete, wakati wa sherehe za maadhimisho hayo, jijini Dar es Salaam leo. (Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR)
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maadhimisho hayo.
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikitoa heshima zake, mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maadhimisho hayo.
Kikosi cha Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), kikitoa heshima zake, mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maadhimisho hayo.
Kikosi cha Jeshi la Magereza, kikitoa heshima zake, mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maadhimisho hayo.
Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha halaiki, wakionesha aina mbalimbali ya michezo kwenye maadhimisho hayo.
Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha halaiki, wakionesha mchezo wa sarakasi na maumbo mbalimbali wakati wa sherehe hizo leo.
Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki, wakionyesha sarakasi ya mlingoti wa bendera, wakati walipokuwa wakionesha maumbo mbalimbali wakati kwenye sarakasi hiyo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanzania.
Kikundi cha Sanaa cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) cha Oljoro, kikionesha umahiri wake wa kuimba na kucheza 'Kiduku' , wakati walipokuwa wakiimba kwaya kwenye sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jijini Dar es Salaam leo, Aprili 26, 2012.
No comments:
Post a Comment