TANGAZO


Thursday, April 12, 2012

Serengeti Breweries yazindua Smirnoff Ice

  Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya serengeti bwana Ephraim Mafuru katika akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kinywaji kipya cha kampuni hiyo SMIRNOFF  ‘ ICE’ kilichozinduliwa rasmi siku ya jumamosi katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar, kulia ni meneja wa vinywaji vikali wa kampuni hiyo bwana Emilian  Rwejuna,(kushoto) ni meneja  wa SMIRNOFF   ICE  Bi  Azda  Amani. (Picha na Mpiga picha Wetu)

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya serengeti bwana Ephraim Mafuru katika akiielezea kinywaji  kipya cha kampuni hiyo SMIRNOFF  ‘ ICE’ kilichozinduliwa rasmi siku ya jumamosi katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar, kulia ni meneja wa vinywaji vikali wa kampuni hiyo bwana Emilian  Rwejuna,(kushoto) ni meneja  wa SMIRNOFF   ICE  Bi  Azda  Amani.


UZINDUZI WA SMIRNOFF ICE
Na Mwandishi wetu
Ephraim Mafuru na Meneja wa Smirnoff Ice, Azda Amani
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries  (SBL), hivi karibuni imeingiza kinywaji kipya sokoni cha SMIRNOFF ICE, ambayo inatengenezwa na kusambazwa na kampuni hiyo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ofisi za kampuni hiyo Oystabay jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo bwana Ephraim Mafuru , amesema SBL imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu mojawapo ya kutimiza mahitaji ya wateja wake na kuwa karibu zaidi na wateja, wadau na wapenzi wa bidhaa ziazozalishwa na kampuni hiyo.
“Hapo awali tumekuwa tukisambaza kinywa chetu cha SMIRNOFF  SPIRIT, kinywaji kikali ambacho kwa watumiaji wengi ni lazima wachanganye na kinywaji kingine kama soda au juice ili waweze kukinywa lakini sasa tumeamua kuwasaidia wale wateja wetu wanaopenda mchanganyiko huo kwa kuwatengezea SMIRNOFF ICE   ambao ina mchanganyiko wa limao na ndimu” alisema Mafuru.
Kwa upande wake Meneja wa vinywaji vikali (spiti brand manager) Bwana Emilian Rwejuna amesema kuna aina mbili za SMIRNOFF ICE , ambapo SMIRNOFF ICE black ina mchanganyiko wa vodka na ndimu na SMIRNOFF ICE red ina mchanyiko wa vodka na limao itakoyowasaidia wateeja wetu wanaopenda kutumia vinywaji vikali vyenye mchanganyiko wa ndimu na limao kupunguza kazi ya kuchanganya vinywaji hivyo na badala yake wapate kinywaji kikiwa  kimechanganywa tayari kwa kutumia.
“Wateja wetu wengi  wanaopenda kutumia SMIRNOFF wanapenda kuchanganya  kinywaji hicho na vinywaji vingiune kama soda, limao, ndimu, na barafu lakini sasa tumetengeza SMIRNOFF ICE ambayo tayari imeshachanganywa na inaruhusiwa kuwekwa kwenye jokofu ili inywewe ikiwa ya baridi” alisema Rwejuna.
Naye meneja wa brandi ya SMIRNOFF ICE , Bi  Azda  Amani amesema kinywaji hicho kinaweza kutumiwa na watu wa jiansia zote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea huku akisisitiza kuwa vinywa vyote vyenye kile vinavyotengenezwa na SBL haviuzwi kwa watu wenye umri chini ya miaka 18 na kuwataka wale wenye sifa ya kutumia vinywaji hivyo wanywe kistaarabu. 

No comments:

Post a Comment