TANGAZO


Wednesday, April 11, 2012

Sudan yaapa kurejesha visima vyake

Mapigano kwenye mpaka Sudan na Sudan Kusini

Sudan imeapa kutumia "mbinu zote halali" kuyatimua majeshi ya Sudan Kusini kutoka kisima chake kikubwa cha mafuta,kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la habari la taifa Suna .
Vikosi vya Sudan Kusini viliteka eneo la Heglig siku ya Jumanne huku mapigano makali yakiendelea kwa siku ya pili mfululizo.
Pande zote mbili zinalaumiana kuchochea mapambano katika eneo la mpaka linalogombewa lenye utajiri wa mafuta.
Mapambano makali katika kipindi cha wiki mbili zilizopita yamezusha wasiwasi wa kurejea kwa vita kamili kati ya pande hizo mbili.
Eneo la Oil-Heglig lenye utajiri mkubwa wa mafuta kwa jumla linatambuliwa kuwa ni sehemu ya kaskazini ingawa Sudan Kusini inabisha hilo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Sudan inasema itatumia kila mbinu halali kukabiliana na uchokozi wa Sudan Kusini .
"Serikali ya Sudan inatangaza baada ya shambulio hili kwamba itachukua kila hatua zinazolazimika na kuonya "maangamizi" upande wa kusini.
Taairifa hiyo pia ilionya kuwa "uchokozi wa taifa hilo jipya hautasaidia chochote ila kuwaletea uharibifu na majonzi kwa watu wake".
Msemaji wa kijeshi wa Sudan Kusini Philip Aguer amesema eneo la kusini linashikilia kisima cha mafuta cha Heglig.
Alisema wanajeshi walisonga mbele hadi Heglig baada ya kushambuliwa na wanajeshi wa Sudan kutoka angani na nchi kavu.

No comments:

Post a Comment