TANGAZO


Monday, April 23, 2012

Rais Shein, mkewe, washiriki zoezi la kupiga picha za vitambulisho vya Taifa, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiwa katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi kushiriki katika zoezi la upigaji picha za vitambulisho vya Taifa, mjini Zanzibar leo, sambamba  na utiaji saini fomu maalum na kuweka  alama za vidole, ikiwa ni utaratibu  wa ukamilishaji wa zoezi hilo.  Aliyesimama kushoto ni  Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa Zanzibar, Vuai Mussa Suleiman.  (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati)  akiweka  alama za vidole, baada ya kupiga picha za vitambulisho vya Taifa, sambamba na utiaji saini fomu za ukamilishaji wa zoezi hilo. Zoezi hilo lilimefanyika leo katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi, Mnazi mmoja, mjini Unguja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa, Zanzibar, Vuai Mussa Suleiman. Kulia ni Mathayo Msungu wa NIDA. 

No comments:

Post a Comment