TANGAZO


Wednesday, April 4, 2012

Rais Shein awaapisha Mawaziri Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri aliowaapisha waliosimam, hafla hiyo iliyofanyika leo mjini  Ikulu Mjini Zanzibar, wengine ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff (kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kulia). (Picha
na Ramadhan Othman Ikulu)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha  Ramadhan Abdalla Shaaban, kuwa Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,  kabla Shaaban, alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali. 
 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein, akimuapisha Ali Juma Shamhuna, kuwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo, kabla Shamuhuna, alikuwa Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati.
 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Suleiman Othman Nyanga, kuwa Waziri wa
Kilimo na Maliasili, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
leo, kabla Nyanga, alikuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri
asiyekuwa na Wizara Maalum.
 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Abdilah Jihad Hassan, kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, leo Ikulu Mjini Zanzibar, kabla Jihad alikuwa Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo.

No comments:

Post a Comment