TANGAZO


Wednesday, April 4, 2012

Mama Tunu Pinda, awataka Watanzania kuisaidia Taifa Queens


 Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, akimkaribisha mgeni wake, mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Tunu Pinda, mara baada ya kuwasili mapema leo asubuhi kwenye ofisi hizo.
 
 
 Mama Tunu Pinda, akiwa ni mmoja wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali, ambaye wameamua kushiriki kuihamasisha jamii na wadau mbalimbali, kuisaidia timu ya mpira ya wanawake ya Netboli (Taifa Queens ), kuhakikisha inafanikisha malengo yake na pia kuhakikisha maandalizi yote yanakwenda sawa. Pichani Mama Tunu Pinda, akizungumza leo kwenye kipindi cha Power breakfast, kupitia Radio Clouds FM, jijini Dar kuhusiana na mchakato mzima wa kuisadia Taifa Queens. Kulia ni mtangazaji Paul James a.k.a PJ wa Radio. (Picha na mpigapicha wetu)


Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (pili kulia), akiwa amepozi katika picha ya pamoja na Watangazaji wa kipindi cha Power breakfast, kutoka Clouds FM mapema leo asubuhi. Mama Pinda alifika kwenye ofisi za Radio hizo kwa ajili ya kuihamasisha jamii kuisaidia timu ya Taifa Queens kwenye michuano yake inayotarajiwa kuanza hivi karibuni hapa jijini Dar. Kutoka kulia ni Gerald Hando, Barbra Hassan pamoja na Paul James.

No comments:

Post a Comment