Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Balozi Raphael Lukindo, Sinza jijini Dar es Salaam leo, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jumanne tarehe 27, Machi na kuzikwa Ijumaa tarehe 30, Machi katika makaburi ya Kinondoni jijini. Marehemu Balozi Lukindo aliyestaafu mwaka 1988, aliitumikia Serikali katika balozi mbalimbali nje ya nchi, ikiwemo Japan, Urusi, Poland, Hungary na Czechoslovakia. Marehemu ameacha mjane na watoto wanne. (Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akimfariji Bibi Tereza Mvaa Lukindo, mke wa marehemu Balozi Raphael Lukindo, wakati Rais alipokwenda nyumbani kwa marehemu, Sinza jijini Dar es Salaam leo, kuwapa pole ndugu na jamaa kutokana na kifo cha Balozi huyo, aliyezikwa juzi Ijumaa katika makaburi ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment