Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Prof. Bingu wa Mutharika, kijijini Ndata, wilyani Thyolo, nje ya jiji la Blantyre, nchini Malawi leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa Marehemu Rais Wa Malawi Bingu wa Mutharika, Bi Calista Mutharika wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwa marehemu Ndata,Wilayni Thyolo, nje ya jiji la Blantyire, Malawi leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Profesa Bingu wa Mutharika, wakati wa mazishi yaliyofanyika shambani kwa marehemu Ndata, wilayani Thyolo leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Profesa Bingu wa Mutharika, baada ya kuweka shada la maua katika kaburi hilo.
No comments:
Post a Comment