TANGAZO


Monday, April 23, 2012

Nape akutana na ujumbe wa wanafunzi kutoka Marekani

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akizungumza wakati wa kikao chake na Ujumbe wa wanafunzi kutoka Marekani waliotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, leo. Nape alizungumza nao masuala mbalimbali yakiwemo ya  Siasa. Kushoto ni Kiongozi wa msafara huo, Jola Yoder kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Spokane, nchini Marekani. (Picha na Bashir Nkoromo)




Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akionyesha kijitabu cha Kilimo Kwanza' wakati wa kikao chake na Ujumbe wa wanafunzi kutoka Marekani waliotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam, leo. 




Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akimkabidhi vitabu vya Kilimo Kwanza' Mkuu wa msafara wa Ujumbe wa wanafunzi kutoka Marekani, Jola Yoder kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Spokane, Marekani, baada ya mazungumzao na ujumbe huo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam, leo. 




Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akimkabidhi 'opener' za CCM, Mkuu wa msafara wa Ujumbe wa wanafunzi hao, Jola Yoder kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Spokane, Marekani, wakati wa mazungumza na ujumbe huo leo Ofisini hapo. 






Kiongozi wa msafara wa wananfunzi kutoka Marekani, Jola Yoder kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Spokane, nchini humo, akimshukuru Nape, baada ya mazungumzao na ujumbe wa wanafunzi hao, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. 






 Nape na kiongozi wa ujumbe wa wanafunzi wa Marekani, Jola Yoder, kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Spokane, nchini humo, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi hao, baada ya mazungumzao yao, yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, leo. 





Nape akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Marekani waliofika Ofisi ya Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, leo.

No comments:

Post a Comment