TANGAZO


Monday, April 23, 2012

Lulu afikishwa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam

 Askari wa Jeshi la Polisi na Magereza, wakiwa katika ulinzi mkali wakati msanii wa maigizo, Elizabeth Michael, jina la kisanii  'Lulu', alipofikishwa Mahakama ya Kisutu, kwa ajili ya kusomewa mashtaka ya kudaiåwa kumuua msanii mwenzake, aliyekuwa akishirikiana naye katika michezo ya maigizo na pia kuhisiwa kuwa mpenzi wake, Steven Kanumba. (Picha zote na Dande Junior)




 Elizabeth Michael, 'Lulu', (mwenye nguo nyekundu), akiwa amewekwa katikati ya askari wa Jeshi la Magereza, alipoletwa Mahakamani hapo kusikiliza shitaka la kudaiwa kuua.
åå


 Lulu, (mwenye nguo nyekundu), akiongozwa kupelekwa kwenye chumba cha Mahakama hiyo na askari wa Magereza wa kike kwa ajili ya kusomewa shitaka lake hilo.



 Lulu, (mwenye nguo nyekundu),  akiwa amezungukwa na askari hao, akipandishwa kwenye jengo la Mahakama hiyo, leo asubuhi.




 Lulu, (mwenye nguo nyekundu),  akiwa katikati ya askari hao, kuelekea kwenye chumba cha Mahakama.




 Lulu, (mwenye nguo nyekundu),  akiwa katikati ya askari Magereza, ameshikiliwa mkono, akiongozwa kuelekea kwenye kizimba cha Mahakama hiyo.



 Wapigapicha wa Vyombo mbalimbali vya habari, wakijitahidi kupata picha za Lulu, aliyewekwa katikati na askari hao na hivyo kusababisha usumbufu wa kupatikana picha zake kwa usahihi.




 Lulu akiwa katikati ya askari hao, walioweka ulinzi mkali kwa msanii huyo.




 Lulu, akishuka ngazi za jengo la Mahakama hiyo, baada ya kusomewa shitaka lake hilo.




 Askari Polisi wa Mahakama, akimuongoza Lulu, kuelekea kwenye gari la askari Magereza kwa ajili ya kurejeshwa mahabusu.




Askari Polisi na Magereza, wakiwa sambamba na Lulu, wakimuongoza kuelekea kwenye gari la Magereza.



 Kila kona ya Mahakama ya Kisutu, hali ya ulinzi ilikuwa imara kwa ajili ya kulinda usalama Mahakamani hapo.




 Gari lililomleta Lulu, likiwa kwenye viwanja vya Mahakama hiyo, likimsubiri.




 Baadhi ya waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali pamoja na wananchi waliofika kwenye Mahakama hiyo, wakitoka nje baada ya kesi hiyo ya Lulu kusomwa.

No comments:

Post a Comment